Watu wa Makete hutumia mbegu za Marijuana kukaangia chakula tangu zamani
Huku harakati za kutaka matumizi
ya Bangi kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani,
Tanzania haijaachwa nyuma.
Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa
Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka serikali iweke sheria
ambayo itaweza kuhalalisha matumizi ya mmea huo.
Wanakijiji hao zamani walikuwa
wakitumia mbegu za mmea huo kukaanga na chakula lakini siku hizi
wanalazimika kuzitumia kwa usiri mkubwa wakihofia kukamatwa na polisi.
Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete
Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza
leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi
kukaanga na chakula.
Na kama mmea huo ungekuwa na hatari kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa.
SOURCE: BBC
Post a Comment
Add comment