RAIS Jakaya Kikwete amesisitiza nia ya Serikali kutumia wahitimu wake wa vyuo vikuu, kufundisha shule za msingi huku akiwaweka sawa kwa kuwaambia kufanya hivyo si kuwashushia hadhi. Hatua hiyo ya walimu wenye Shahada kuanza kufundisha shule za msingi tofauti na ilivyozoeleka, chini ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, ni sehemu ya mageuzi makubwa, yanayotarajiwa kufanyika katika sekta ya elimu nchini.
Rais
Kikwete alishawahi kutamka mpango huo wa kutumia wasomi wa vyuo vikuu
katika shule za msingi, kutokana na idadi kubwa ya wahitimu wa ualimu,
kutarajiwa kuwa kwenye soko la ajira.
Alisisitiza
kuwa baada ya mwaka, wahitimu wa vyuo vikuu watafundisha katika shule
hizo na kwamba kufanya hivyo si kuwashushia hadhi.
Post a Comment
Add comment