
Askofu mstaafu wa Afrika Kusini Desmond tutu amesema
kwamba anaunga mkono wagonjwa mahututi wanaotaka kusaidiwa kufariki
wafanyiwe hivyo.
Akiandika katika jarida la 'The Observer'',alisema yeye anasheshimu utu lakini hali inaweza kubadilika.
Pia alisema kuwa kuendeleza maisha ya Nelson Mandela ilikuwa kumvunjia heshima.
Maoni ya askofu huyo mstaafu wa kanisa la
kianglikana, ni sawa na yale aliyetamka Askofu mkuu wa kanisa la
'Canterbury Lord Carey' ambaye pia aliunga mkono usemi huo.
Kanisa la kianglikana limeagiza uchunguzi kuhusu jambo hili.
Akiandika katika jadrida hilo, askofu huyu
mstaafu wa kanisa la Anglikana Afrikakusini na mwenye miaka themanini na
mbili alisema kwamba ''iwapo twahitaji mashine za kupumua,bila shaka
tunahitaji kuuliza ubora wake na vile fedha zinavyotumika.''
Vile vile alieleza kuwa ni aibu vile aliyekuwa
kiongozi wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliwekwa hai kwa mda mrefu
hospitalini katika hatua za mwisho za maisha yake huku akipigwa picha na
wanasiasa waliomtembelea.
Amesema kuwa Madiba hakujielewa kwa lolote na tendo lao lilikuwa ukiukaji wa heshima za hayati Mandela.
'Ni kweli kwamba watu watahuzunika iwapo nitasema nisaidiwe kufa lakini kwa kauli yangu binafsi sina shaka na hilo.''
Tutu aliandika kuwa,hata ingawa amebadilisha
maoni yake,uhakika wa hapo awali hautiliwi maanani kwenye uhalisia wa
mambo yalivyo a hasa kwa wagonjwa walio mahututi.
SOURCE: BBC
Post a Comment
Add comment