Memba wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhan ’Tunda Man’
amekutwa na mauzauza baada ya kupokea simu yenye namba zinazodaiwa kuwa
za ajabu na kumsababishia atokwe damu puani, mdomoni na kupooza upande
mmoja.
Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo ambacho kilikuwa ndani ya
Hospitali ya Palestina ambako Tunda Man alilazwa, kimeeleza kuwa, tukio
hilo lilitokea mwanzoni mwa wiki hii wakati staa huyo akifuturu.
“Alipigiwa na namba f’lani hivi ya ajabuajabu inayoishia na 39 kama
mara 30 hivi, hakuipokea maana alishawahi kusikia juu ya namba za ajabu
lakini baadaye akaamua kupokea ndipo ghafla akaanguka, akaanza kutokwa
damu puani kisha kuzimia kabisa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Tulimfikisha Hosptali ya Palestina na hali yake ilikuwa mbaya sana
lakini kwa jitihada za madaktari na manesi wamemsaidia kwa sasa kidogo
anaendelea vizuri.”
Tundaman anasema,
“Nakumbuka nilipokea simu yenye namba nisizozifahamu ambayo iliita
sana nikajishtukia kuipokea lakini baadaye nikahisi ni kama namba za nje
ya nchi labda ni dili la kwenda kufanya shoo, nilivyopokea tu sikuwa
nasikia mtu akiongea zaidi ya kusikia mtu kama vile anapuliza kitu.
“Baada ya hapo nikajiona naishiwa nguvu, damu zikinitoka puani na
mdomoni kisha nikajikuta nipo Hospitali ya Palestina,” alisema Tunda
Man.
Post a Comment
Add comment