GuidePedia

0
Mtoto wa pekee wa Jackie Chan Jaycee mwenye miaka 30 amepata changamoto toka kwa baba yake baada ya kuambiwa hatorithishwa mali yoyote na baba yake staa wa filamu ulimwenguni Jackie Chan.
Awali Jackie Chan alidai kumpatia mwanae nusu ya mali zake na nusu nyingine kuitoa kama msaada katika vituo  vya kulelea watoto, lakini alibadili uamuzi wake na kusema kuwa mwanane uyo hatapata mali yoyote kutoka kwake bali ataitoa yote katika vituo vya kulelea watoto yatima.
 
Jackie Chan amemuhasa mwanaye kuwa ni lazima ajitume ili kupata mali zake mwenyewe na hasimtegemee yeye zaidi, Jaycee mpaka sasa ameshacheza filamu 20 toka mwaka 2004.

Post a Comment

Add comment

 
Top