Pamoja na kuwa waongozaji wa video wa Bongo wanafanya kazi nzuri lakini dharau na mapozi ndivyo vilivyomkimbiza Diamond na kuamua kufanya video na waongozaji wa nje.
Diamond alifunguka wakati akihojiwa na Vanessa Mdee mtangazaji wa kipindi cha Hitlist cha Choice FM Diamond alidai kuwa waongozaji wa video Bongo wana mapozi na dharau kiasi kwamba unaweza ukamlipa pesa alafu bado akawa haoni uthamani wako, kwani wengi wao wamekuwa na maringo na kupenda tabia ya kuwapiga kalenda wasanii.
Diamond aliongeza pia kuwa alishindwa kufanya video ya Lala Salama, Nimpende Nani kwa sababu Mwongozaji alikuwa akimpiga kalenda ilihali alikuwa keshalipia video zote mbili, ivyo Diamond akaamua kususia Waongozaji wa video nchini.
Post a Comment
Add comment